Follow by Email

Tuesday, October 2, 2012

Viongozi wa Tume ya Mipango na Wizara ya Mambo ya Nje wakutana jijini DarKatibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa John Haule (aliesimama) akiwakaribisha Wajumbe kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa ajili ya kuasilisha mada kuhusu Mfumo wa Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa leo tarehe 02 Oktoba 2012.


Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliesimama) akiwasilisha mada katika mkutano wa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu Mfumo wa Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo tarehe 02 Oktoba 2012.
Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Mhandisi Hapiness Mgalula (Miundombinu na Huduma) aliyesimama kushoto akijitambulisha katika mkutano wa Mfumo wa Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango ya Maendeleo ya Taifa katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo tarehe 02 Oktoba 2012.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.